kwamamaza 7

Kusini:Utalii waingizia frw miliyoni 23 kipindi cha miezi mitatu

0

Wilaya za Huye na Nyanza,kusini mwa nchi ni miongoni mwa wilaya zenye historia kubwa nchini Rwanda,ambazo zimekuwa  kivutio kikubwa kwa watalii kutoka nje na hata wananchi kutoka maeneo mbali mbali nchini.

Kwa muda wa miezi mitatu iliyopita tayari wilaya hizo mbili zimekusanya zaidi ya  frw milioni 23 ikiwa ni pamoja na mapato yanayoingia kutokana na utalii wa ndani.

Mkuu wa wilaya ya Nyanza,Erasme Ntazinda  ameleza   kuwa kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita kiwango cha watalii kimefikia idadi ya watu 23,000 hadi 45,000 mwaka 2017.Ameongeza kuwa idadi ya wakazi wa Nyanza wanaotembelea maeneo ya kihistoria idadi kubwa ni vijana na wanafunzi kwa ujumla.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Diwani Ntazinda amendelea kusema   kwamba hatua zinachukuliwa ili kuweza kuweka vivutio zaidi ili watalii waweze kuvutiwa na kuingiza kipato kwa kiwango cha juu.

“Kwa kushirikiana na RDB tunataraji kukusanya taarifa zote za muhimu kuhusu historia ili watalii waweze kujua zaidi historia ya Rwanda na hivyo kuweza kuwa vivutio zaidi”.

Sehemu muhimu za kihistoria ni pamoja na jumba la kihistoria lilipo katika wilaya ya  Huye, Nyanza Murukali,Bugeni wilayani Nyanza na kwa Nyagakecuru wilayani Huye.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Safari John Bosco mkurugenzi katika jumba la makumbusho wilayani Huye,amesema kuwa hatua kubwa imepigwa na kwamba kuna mipango madhubuti ya kuboresha maeneo yote ya kihistoria ili kuongeza zaidi mapato kupitia sekta ya utalii katika wilaya ya Huye na Nyanza.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Ama kuhusu kuboresha maeneo hayo ya kihistoria,katibu mkuu mtendaji wilaya ya Huye Vedaste Nshimiyimana Vedaste amesema kuwa hadi sasa wilaya ya Huye kwa kushirikiana na kitengo cha utalii RDB,tayari kuna mpango wa kujenga mahoteli na migahawa katika maeneo ya kihistoria ili kuyafanya maeneo hayo kuwa kivutio zaidi.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Hassan Thabiti/Bwiza.com

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.