HABARI MPYA

Kuna waovu lakini haina budi kuwazuia popote watokapo-Rais Kagame

Rais wa Rwanda,Paul Kagame akianzisha mwaka mpya 2018,amewashukuru Wanyarwanda ushirikiano mnamo mwaka 2017 na kuwakumbusha kuna waovu wanaotaka kuharibu waliyotimiza na kwamba haina budi kuwazuia popote watokapo.

Rais Kagame amewataka wakazi kuendelea kushirikiana ,kujifunza na kujenga uwezo wa kulinda yale yote waliyotimiza.

Rais Kagame amesema”Kuna waovu,haina budi  kuwazuia popote watokapo,mbinu  zote wanazotumia,hii ni ajili ya kujenga uwezo”.

Rais Kagame amesisitiza kwamba ilionekana waziwazi kuwa ushirikiano ni kiini cha kutimiza mengi kwa Wanyarwanda na kwa hiyo inabidi kutilia mkazo hili jambo milele.

Rais Paul Kagame amewatakia heri na fanaka katika mwaka mpya na kuwakumbusha Wanyarwanda  hasa vijana kuwa lengo la kujenga nchi linamhusu yeyote.

Hotuba yake Rais Paul Kagame

onyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Maombe
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Most Popular

To Top