kwamamaza 7

Kirehe: Wananchi wapewa amri ya kuhama mashamba inayosemekana kuwa mali ya serikali

0

Raia wa Kirehe walalamika kuwa mamlaka ya tarafa ya Mushikiri imewapa amri ya kuhama mashamba ambayo wanaishi na wanayo miliki kwa kupewa na wengi wao wamerithi kutoka wazazi na mababu na wengine kwa kununua.

Wananchi  hawa wemesema kuwa wamerithi ardhi hii kutoka kwa wazazi wao na mababu yao hapo miaka ya 1987 na wakapanda miti ambayo haina uhusiano wowote na kimsitu kingine cha serikali.

Licha ya serikali kudai kuwa mashamba hayo ni mali yake, wananchi hawa wasema kuwa wamekuwa wakiuziana ardhi kati yao na huku serikali ikikaa bila kufanya kitu.

Mmoja wa wananchi, Mukasine Gaudiose aliyenunua ardhi na kupewa vitambulisho amesema “ Nilikuwa nikaishi kwenye makazi yenye hatari, na baada ya serikali kuhamasisha watu kuhamia kwenye maeneo salama karibu na wengine nilikuja hapa nikanunua ardhi kwa faranga elefu 30 ambayo tulifanya hati ya makubaliano na kutiwa sahihi na kiongozi wa kijiji na baadaye tukapewa cheti cha kujenga kutoka tarafa, sasa hivi ikiwa ni siku nyingi tukiishi hapo mamlaka ya tarafa ilituendea ikaomba kuhama mashamba haya kwa kudai kuwa ni mali ya serikali na kutisha kwamba tusipohama watazibomoa nyumba zetu. Kwa hivyo tunaomba serikali kututendea haki kwa sababu hili ni shamba ambalo tulijinunulia pekee.

Licha ya madai ya raia hao kuwa wanatofautiana na uamuzi wa mamlka ya tarafa unaowaamrisha kuhama makazi yao kwa kuwa ni mashamba hayo ni miliki ya serikali, viongozi hao walisema kwamba ardhi hiyo ni mali ya serikali. Kwa mjibu wa Katibu mtendaji wa tarafa ya Mushikiri habari za kuwa ardhi hiyo ni mali ya serikali zilitolewa na washauri wa tarafa.

“mashamba yale ni mali ya serikali ikiwa kuna wananchi waliopewa ni kwa ajili ya kuwakopa ili waweze kuendesha shughuli zao kwa muda lakini kulingana na taarifa kutoka kwa halmashauri ya tarafa mashamba hayo ni milki ya serikali” asema katibu huyo.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Aliendelea kusema kwamba wamewapa muda wakuzihamisha shughuli zao zinazoendeshwa kwenye mashamba hayo kwa kuwa ni mali ya serikali. Tuna wajibu wa kuhakikisha sheria zinaheshimiwa na kwa  kuwa wamekiuka sheria watashurutishwa kuhama na ikiwa kuna yeyote atakayeathiriwa na kauli hiyo kutatafutwa mbinu ya kumsaidia.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Richard Wa Billy

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.