kwamamaza 7

Kiongozi wa wanamgambo afichua alivyosaidiwa na Uganda pamoja na Burundi

0

Msemaji wa kundi la wanamgambo wa FLN, Callixte Nsabimana maarufu kama Sankara ameibuka na kusema kwamba Ugandana Burundi walimpa msaada katika vitendo vyake vya kijeshi.

Sankara,37, ambaye ni mwanasheria amefichua kwamba alimkuta mkuu wa upelelezi wan je nchini Burundi, Meja Bertin maarufu kama Moses ili kuzungumza namana ya kukutana na wanamgambo wa Kanali Kanyemera kushambulia Rwanda.

Mkutano huo, ulikuwa ukilenga namna ya kukutana na Kiongozi wa Upelelezi wa Jeshi nchini Uganda (CMI), Brig. Abel Kandiho.

Amesema kuwa alikutana na Kandiho kupitia rafiki yake, Capt. Charles Sande kama alivyoshauriwa na Mej. Bertin.

Baada ya mkutano, kiongozi mwingine katika chama cha wanamgambo, Bernabe Sinayobye alikwenda nchini Uganda kuomba msaada wa kidiplomasia kwa kuishambulia Rwanda.

Pamoja na hayo, Sankara ameomba msamaha na kwa Wanyarwanda kwa ujumla na kukubali mashtaka yote 16 yakiwemo vitendo vya kigaidi.

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.