kwamamaza 7

Kiongozi afichua marais wa kwanza wa Rwanda walikuwa si raia wake

0

Kiongozi wa Tume ya Kupambana na Mauaji ya Kimbali nchini Rwanda, Dk. Jean Damascene Bizimana amesema Rais wa kwanza wa Rwanda, Gregoire Kayibanda na wa pili, Mej. Jen. Juvenal Habyarimana walikuwa si raia wa Rwanda.

Amefunguka hayo, Wilayani Nyanza kwa kusema marais hao walikuwa wakiwatesa Watutsi juu ya madai kwamba si Wanyarwanda. Amesema historia inaonyesha kwamba hao marais walikuwa na asili nyingine.

Amesema baba yake Kayibanda, Nkangura alikuwa ni mzaliwa wa Bukavu, nchini DRC.

Nkagura alihamia nchini Rwanda mwaka 1915 kwa kutafuta kazi kisha akaishi Kabgayi.

Pia amesema baba wa  Rais Habyarimana, alizaliwa nchini Rwanda lakini asili ya baba yake, Ntibazirikana ni nchini Uganda.

Amesisitiza asili yao iliwafanya kushindwa kuimarisha umoja wa Wanyarwanda kwani walikuwa hawajui wanavyoishi Wanyarwanda tangu zamani za kale.

Dk Jean Damascene Bizimana

Rais Kayibanda aliongoza Rwanda tangu mwaka 1962 baada ya uhuru hadi 1973.

Rais Habyarimana aliongoza Rwanda kutoka mwaka 1973 hadi 1994 baada ya ndege aliyokuwemo kudunguliwa na watu ambao kila upande husema yake.

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.