Connect with us

HABARI MPYA

Kila mmoja hana budi kukiri-Maafisa wa upelelezi wa Uganda

Published

on

Mmoja mwa waliofungwa na kuteswa kimwili na maafisa wa upelelezi wa Uganda(CMI),Fidele Gatsinzi ametangaza kwamba ni lazima kukiri mashtaka yote wanayomshtaki fulani maafisa wa upelelezi wa Uganda kufuatia kuteswa kimwili.

 Mnyarwanda,Fidele Gatsinzi

Akisimulia kisa hiki kwa Virunga Post,Fidele Gatsinzi ameeleza kuwa mafisa wa upelelezi wanawapiga mno wafungwa ili wakiri hata na yale ambayo hawayajui kuhusu   ili wasiendelee kupigwa kiunyama.

Pia ameweka wazi kwamba kuna chumba cha kuwatesea kimwili wilayani Mbarara ambacho ni nadra kuondoka kwa yeyote  akiwa hai kwa kuwa ni kama nyumba ya kuchinjia watu.

Fidele Gatsinzi amesema”Ni kama nyumba ya kuchinjia,hakuna mmoja anayeondoka akiwa hai(…)”.

Pia Gatsinzi ameeleza kwamba chumbani hiki kuna wafungwa wengi ambao walivunjika mifupa,damu ikitililika mwili mzima,ambao wanaishi kwa kupiga mayowe ya usiku mchana na kuongeza kwamba wanachokifanya mafisa wa CMI ni kuwapiga mateke mgongoni,kuwabisha matusi na kuwakemea kwa kupiga kelele.

Bw Fidele Gatsinzi alikamatwa na mafisa wa upelelezi kwa kushtakiwa kuwa mpelelezi wa Rwanda nchini Uganda, alipoenda kumtembela mwanawe ambaye ni mwanafunzi chuoni nchini humo.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

Maombe
Advertisement
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *