kwamamaza 7

Kijana,23, afungwa kwa kutuhumiwa kumbaka bibi yake wa miaka 86

0

Kijana, 23, mkazi wa tarafa ya  Rurenge wilayani Ngoma mashariki ya Rwanda amefungwa jela kwa kutuhumiwa kumbaka bibi yake wa miaka 86.

Katibu Mtendaji wa Tarafa ya Rurenge, Gilbert Mapendo amehakikisha hizi taarifa kwamba huyu kijana amekamatwa baada ya bibi yake kujulisha uongozi kisa hiki.

Amesema” Bibi ndiye ambaye amekuja kumuambia kiongozi wa kijiji kuhusu hili tukio, alikuwa amevimba kwenye shingo kama ishara ya kuwa wamepambana kisha  huyu bikizee akashindwa”

Huyu Kiongozi amehakikisha huyu kijana anajulikana kwa maovu kwani siku zilizopita alifungwa kwa matumizi ya dawa za kulevya.

“ Tunadhani kwamba alikuwa amelewa dawa za kulevya kwani siyo mala ya kuanza,Anajulikana kwa tabia mbaya” Mapendo ameongeza

Ofisi Kuu inafanya upelelezi kuhusu hili na bibi  angali hospitalini kwa matibabu.

Sheria zinaeleza kwamba huu uhalifu unadhibiwa kufungwa kutoka miaka saba  hadi kumi na faini ya frw frw laki tatu hadi miliyoni moja.

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.