HABARI MPYA

Kigali:Watoto waelezea viongozi changamoto zao

Watoto kutoka maeneo mbalimbali nchini pamoja na wengine wa kutoka kambi za wakimbizi karibu 448 wameweka kazi changamoto zinazokumba maisha yao kama vile kazi za sulubu,kuacha shule na mengine.

Kupitia mkutano wa kila mwaka kwa mala ya 12 jana, watoto wamesema kuwa kuna wenzao walioacha shule kisha wakaanza kufanya kazi za nguvu kama vile kwenye mashamba ya chai,kuwa madobi na mengine.

Pia watoto hawa wameuliza kwa nini serikali ilitaka kupunguza idadi ya watoto wanaoacha shule lakini serikali hufukuza wanafunzi waliokaribu kufanya mitihani ya taifa juu ya kosa dogo.

Katibu hali wa wizara ya elimu,Isaac Munyakazi amejibu kuwa isipokuwa kosa la kuwa na itikadi ya mauaji ya kimbali,haifai kufukuza mwanafunzi kwa makosa ya kawaida kwani baadhi ya wajibu wa wizara ya elimu ni kulinda haki za watoto wa nchi.

Waziri mkuu,Edouard Ngirente akianzisha mkutano huu ameleza kuwa idadi kubwa ya wananchi ni vijana na kwa hiyo haina budi kupambana na ukiukaji wa haki za watoto hasa kuwapachika mimba waschana wenye umri mdogo.

Takwimu za mwaka 2012 zilionyesha kuwa watoto chini ya miaka 15 ni 42%.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Maombe
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Most Popular

To Top