HABARI MPYA

Kigali:Wanachama wa FDU-Inkingi wahukumiwa kufungwa mwezi kizuizini,mmoja achiwa huru

Mahakama kuu ya Nyarugenge imeamua kufunga mwezi kizuizini wanachama saba wa FDU-inkingi wakiwemo kiongozi makamu wake,Boniface Twagirimana na kuachia huru mmoja kwa jina la Erneste Nkubito.

Kiongozi makamu wa chama cha upinzani FDU-Inkingi,Boniface Twagirimana

Hawa wanatuhumiwa kuunda kundi la kijeshi kinyume na sheria kwa jina la P5 eneo la mashariki mwa DR Congo kwa kusajili wanajeshi.

Taarifa za VOA zinasema kuwa watuhumiwa hawakuwa chumbani cha hakimu aliyesoma hukumu kwa kuwa mahakama imeamua kusoma hukumu bila kuwajulisha na hata watangazaji.

Kwa upande wa watuhumiwa wanakana ema mashtaka haya yote kwa kusema kwamba kesi hii ni ujanja wa serikali ya Rwanda kuwafukuza katika uwanja wa siasa.

Boniface Twagirimana alisikika mala nyingi akikosoa serikali ya Rwanda kuhusu mambo mbalimbali hasa siasa.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Maombe
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Most Popular

To Top