HABARI MPYA

Kigali:Serikali kuadhibu wanaovutia sigara hadharani

Viongozi wa mji wa Kigali wameweka wazi kuwa kutatolewa adhabu kwa watu wanaovuta sigara hasa hadharani.

Kupitia mahojiano na watu na mashilika husika na kulinda afya ya binadamu kama vile shilika la kimataifa la afya,WHO diwani wa mji wa Kigali,Pascal Nyamulinda ametangazia VOA kwamba sigara ingali baadhi ya chanzo cha vifo vya watu wengi duniani ikiwemo Rwanda.

Kiongozi huyu amesema kuwa jambo hili litawezekana kwa kuwa waliyaweza kuyatatua mengine yakiwemo usalama na usafi.

Tutatumia nguvu nyingi kwa kufanya kampeni zitakazo dumu kwa kupambana na uvuta sigara hadharani kama vile baani”amesema Diwani Nyamulinda.

Afisa wa shilika la kimataifa la kupambana na uvuta sigara,Joseph Ngamije ameleza kuwa watasaidia mji wa Kigali kupambana na jambo hili na kuwa serikali inaweza kutumia nguvu za wanausalama wakati amabapo wakazi hawafuatilii kanuni.

Pia,wakazi wa mjini Kigali wamesema kuwa uvuta sigara umeisha shamiri mji mzima,madai yanayohusiana na takwimu za utafiti wa serikali mwaka 2013 kuwa asilimia 12 za watu wazima nchini huvuta sigara.

Pamoja na haya waganga huonya watu kuacha uvuta sigara kwa kuwa hili husababisha ugonjwa kadhalika hasa ugonjwa wa kupumua.

Diwani wa mji ametanhgaza haya wakati ambapo wizara ya afya ilitoa sheria ya kuonyesha pahali panaporuhusiwa kuvutiwa sigara.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

Maombe
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Most Popular

To Top