HABARI MPYA

Kigali:Mwendeshamashtaka awatakia wanachama wa FDU-Inkingi kuendelea kufungwa jela

Mwendeshamashstaka amewatakia wanachama watatu wakiwemo Theophille Ntirutwa,Venant Abayisenga na Athanase Kanyarukiko kuendelea kufungwa jela.

Mwanasheria wa washatakiwa Me Gatera Gashabana amekataa ombi hili kwa kueleza kuwa mwendeshamashtaka alichelewa siku moja ya kutoa ombi la uamuzi wa kuendelea kuwafunga watuhumiwa kwa hiyo wangewachia huru,ombi ambalo jaji amekanusha na kueleza kuwa haitazuia kesi kuendelea.

Mwendesha mashtaka ameleza kuwa wanaendelea kufanya upelelezi zaidi kwa hiyo haina budi kuendelea kuwafunga.

Kwa mjibu wa VOA,Watuhumiwa wamekana mashtaka yote kisha wakaeleza kuwa maelezo ya mwendeshamashtaka ni mbinu za chama tawala kuwatesa wanachama wa FDU-Inkingi.

Wanachama wa FDU-Inkingi hawa wanashatakiwa kuunda kundi la kijeshi na kudhamiria kutendea maovu serikali.

Mahakama itatoa uamuzi wake tarehe 5 Disemba 2017.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Maombe
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Most Popular

To Top