HABARI MPYA

Kigali:Mahakama yapiga marufuku tena ombi la Diane Rwigara la kuachiwa huru

Jaji ameleza kuwa mwendeshamashtaka alitoa sababu halali ambazo zinamfanya Diane Rwigara na mama yake,Adeline Rwigara kutoachiwa huru hadi itakapoanzishwa kesi.

Taarifa za The EastAfrican zinaeleza kuwa jaji ambaye jina lake halikutambulika alisema kuwa wanayoshtakiwa Diane Rwigara na mamaye ni nyeti.

Diane Rwigara,35, anashtakiwa kutumia hati bandia kwa kuwania ugombea wa uchaguzi wa rais na uchochezi ,mashataka ambayo hukana kwa kusema kuwa ni kwa ajili ya kutaka kumnyamazisha kwenye uwanja wa siasa nchini Rwanda.

Mamaye,Adeline Rwigara anashtakiwa uchochezi na ubaguzi wa kikabila,naye pia anakanusha mashtaka yote.

Jana mama mzazi wa Diane hakukuja mahakamani,ilisemekana kuwa alikuwa mgonjwa.

Pamoja na haya,Diane Rwigara alishtaki mahakama hii kutokuwa huru kwa kukata kesi  yake vilivyo kwa kueleza kuwa hukumu itatoka ikuluni.

Diane alisema”Najua kwamba hamna uwezo wa kuamua kuniachia huru,najua kuwa uamuzi utatolewa na ikulu,siyo nyinyi”aliwambia baraza la majaji watatu.

Uhalifu wa matumizi hati bandia unadhibiwa kufungwa jela miaka saba wakati ambapo uchochezi ni kufungwa jela kuanzia miaka 10-15 na ubaguzi wa kikabila ni kufungwa jela  kuanzia miaka mitano hadi 10.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Maombe
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Most Popular

To Top