HABARI MPYA

Kigali:Kukamatwa kwadhihirisha kundi la wanamgambo linalodhamiria kupindua serikali ya Rwanda

Baada ya polisi ya Rwanda kukamata watu nane kwa kutuhumiwa kuunda  kundi la jeshi kinyume na sheria,kumedhirishwa kundi kwa jina la Platform Five(P5) lisilokuwa likijulikana kwa wengi nchini  lenye dhamira ya kupindua serikali ya Rwanda.

Mwenyekiti wa FDU-Inkingi,Ingabire Umuhoza Victoire aliye gerezani/Picha:Intaneti

Wanachama cha upinzani ambacho hakijasajiliwa na serikali ya Rwanda, FDU-Inkingi wakiwemo  Gratien Nsabiyaremye, Evode Mbarushimana, Leonille Gasengayire, Boniface Twagirimana, Fabien Twagirayezu, Erneste Nkiko, Papias Ndayishimiye na Norbert Ufitamahoro  wameshtakiwa kushirikiana na P5  kwa maandalizi na kuajiri washiriki wake.

Kwa mjibu wa taarifa za The EastAfrican,kundi hili la P5 linafanyia shughuli zake nchini DR Congo, lilianzishwa mwezi Juni 2016  na linaundwa na chama cha RNC(upande wa Dkt.Eugene Rudasingwa),FDU-Inkingi,PS-Imberakuri(upande wa Bernard Ntaganda,PDP-Imanzi na Amahoro PC.

Vyama hivi vyote havijasajiliwa na serikali ya Rwanda.

Taarifa kutoka mahakama ya Nyarugenge zinasema kuwa  kuna uhusiano kati ya  watuhumiwa na Maj.Faustin Ntilikina,aliyekuwa mwanjeshi kwa uongozi wa Gen.Major Juvenal Habyarimana anayeishi nchini Ufaransa.

Wanasheria wamesema kuwa hata kama P5 haijulikani, kundi hili halina nguvu za kupindua serikali.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

 

Maombe
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Most Popular

To Top