HABARI MPYA

Kigali:Diane Rwigara,nduguye na mzazi wao wakana mashtaka yote

Kesi ya Diane Rwigara,nduguye Anne Rwigara na mama mzazi wao,Adeline Mukangemanyi mahakamani ya Nyarugenge wameweka wazi kutojua wanayoshtakiwa yote.

Diane Rwigara amekana uhalifu wa kutumia hati bandia na kuhusudia kuzusha ghasia nchini.

Sikubali mashtaka haya”amesema Diane Rwigara.

Pia nduguye,Anne Rwigara amekana uhalifu wa kuzusha ghasia nchini kwa kusema kuwa anashangazwa na mashtaka haya na kuwa hakubali.

Mama mzazi wao,Adeline Mukangemanyi amekana madai haya kwa kusema kuwa anashukuru sana ila hakubali anayoshtakiwa na kupendekeza kupata wanasheria wengine wakiwemo Me Gatera Gashabana zaidi ya Me Buhuru Pierre Celestin ili kujua mengi kuhusu kesi hii.

Mwendeshamashtaka ameleza kuwa mahitaji ya Adeline Mukangemanyi ni ujanja wa kupoteza wakati.

Mahakama imeamua kumpa Adeline  Rwigara siku mbili za kujitayarisha.

Kesi itaendelea tarehe 13 Otoba 2017.

Hii ni mala ya tatu kesi hii kuhairishwa.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

 

 

Maombe
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Most Popular

To Top