HABARI MPYA

Kigali:Diane Rwigara,ndugu ye na mama yake wakamatwa na kurudishwa kwao baada ya kuhojiwa

Polisi imekamata Diane Rwigara,nduguye Anne Uwamahoro na mama yake,Mukangemanyi nyumbani kwao kiyovu mjini Kigali ili wahojiwe.

Dianne Rwigara akingizwa garini

Haikuwa rahisi kuingia kwa kuwa imebidi polisi kupanda ukuta na kuwakuta familia hii imejifungia nyumbani.

Askari polisi wakipanda ukuta wa nyumba 

Pamoja na hayo,polisi imetangaza baada ya mda mfupi kuwa familia hii imesindikizwa na kurudishwa kwao baada ya kuhojiwa kuhusuiana na tuhuma za kughushi nyaraka na kukwepa kodi.

Diane Rwigara ni msichana ambaye mwaka huu alitangaza nia ya kugombea urais,ila juhudi zake zilifika upeo baada ya tume ya uchaguzi nchini kufafanua kwamba hakutimiza mahitaji kwa kuwa alitumia kughushi sahihi za watu waliokuwa wameisha fariki.

.Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Maombe
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Most Popular

To Top