kwamamaza 7

Kigali:Mali ya familia ya Rwigara kuuzwa kwa mnada

0

Mkurugenzi wa Ofisi kuu ya kodi(RRA) Richard Tushabe ameweka wazi kuwa serikali itauza kwa mnada mali ya familia ya Rwigara ikiwemo nyumba ya kifahari iliyoko kijijini Kiyovu mjini Kigali,magari na ardhi.

Richard Tushabe amesema kuwa watafanya mnada itakaposhindwa  familia ya Rwigara  kulipa kodi ilizokwepa kulipa tangu mwaka 2012 ambazo ni  $ miliyoni sita kabla ya mwisho wa mwezi Novemba,2017.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Tutaweka sokoni mali yao sokoni watakaposhindwa kulipa kodi kabla ya mwisho wa mwezi Novemba”amesema Tushabe.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Pia, taarifa za The East African zinasema kwamba mkurugenzi wa RRA amesema kuwa wanaweza kuahirisha mnada wakati ambapo familia ya Rwigara inaonyesha mkakati kamili wa kulipa kodi.

Pamoja na haya,Kuna taarifa kwamba benki  zimeanza kushika mali zilizopata kama ankara kwa lengo la kuiuza kwa mnada.

Kwa upande mwingine,wanafamilia ya Rwigara wanaendelea kusema kuwa mashtaka haya ya kukwepa kodi ni yale ya kisiasa.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Mmoja wao,Diane Rwigara alipokuwa mahakamani mwezi uliopita alimuambia hakimu kwamba viongozi walijaribu kumshawishi kutia saini ya mpango wakulipa kodi kwa nguvu.

Diane Rwigara alisema kuwa ni mpango uliokuwa na pendekezo kuwa familia ya Rwiagara inaweza kulipa $miliyoni sita wakati wa mwka mmoja,jambo alilolikanusha mno.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Familia hii inatakiwa kulipa fedha hizi mbali na kufunga kiwanda cha sigara kilichokuwa kiini cha fedha za familia hii.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Kiongozi wa familia hii,Rwigara Assinapol alifariki kwa ajali  mwaka 2015,baadhi ya wanafamilia wengine wakiwemo,mkewe Adeline Rwigara na binti ye, Diane Rwigara wangali gerezani kwa kushtakiwa uchochezi kuzusha ghasia nchini na matumizi ya hati bandia ili kuwania urais.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.