Connect with us

HABARI

Karongi:Ashtakiwa kumuua mkewe kwa kumkata na panga

Published

on

Bahigabose Fidele, mwenye umri wa miaka 39, raia wa Karongi ashtakiwa kumuua mkewe ambaye walikuwa wakiishi pamoja kinyume na sheria.

Katika kesi hii iliyoasilishwa kwa mahakama kuu ya Karongi na uendeshaji mashtaka wa juu wa Karongi, inamshtumu Bahigabose Fidele kumwua mkewe kwa kumkata na panga kichwani usiku wa tarehe 16 Juni 2017.

Maafa haya inasemekana yalitokana na ugomvi kati ya marehemu Mwitirehe Jeanne na Bahigabose Fidele, Huyu alikuwa akitaka fedha kutoka kwa mkewe naye akamwambia kwamba hana, na kumutukana mumewe kwamba ni mbwa na hivyo akamkata na panga. Ilikuwa ni saa tatu za jioni katika kijiji cha Kamina, eneo la Gasiza, tarafa ya Rugabano ya wilaya ya Karongi.

Mtuhumiwa huyu ambaye walikuwa wamezaa watoto wanne alimkata kwa panga kichwani na kumwacha hapo. Usiku uliofuata ndipo watoto walipoamka na kuyiona maiti ya mama wao ikilala hapo sebuleni na wakawaita jirani kwa ajili ya msaada. Mhalifu yeye alikamtwa na yuko kizuizini gereza ya Bwishyura kwa mjibu wa habari kutoka uendeshaji mashtaka wa juu zaidi.

Akipatikana na kosa mhalifu huyu huenda akaadhibiwa kulingana na ibara la 143 ya sheria NO01/2012 la 02/05/2012 linaloziunda kanuni za adhabu.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

 Richard Wa Billy

Maombe
Advertisement
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *