kwamamaza 7

Kampuni ya mawasiliano ya simu za mikononi MTN Rwanda kukabiliwa na mahakama kwa kukosa kumlipa mwananchi fidia.

0

Siku ya jumatano ya tarehe 5 Juni kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi imekuwa mbele ya bunge ikijieleza kuhusu kesi ya kukosa kumlipa fidia mwanaume aliyekipeleka mahakamani kwa mashtaka ya kumharibu.

Mwanaume huyu anayetambulika kama Joseph Ndabakenga iliishtaki MTN Rwanda kumharibu mwili kupiatia mlio wa injini ya kuwasilisha stima kwenye mnara wa mtandao wa MTN Rwanda na hata kuharibiwa na eks rei zake.

Aliiambia mahakama kwamba matokeo ya mitihani ya daktari yalionyesha yaliipata aina ya sumu ijulikanayo kama “Electro-Magnetic Radiation Poisoning”

Kesi hiyi ilipitia mahakama nyingi kuanzia Mahakama ndogo ya Huye na rufaa ikapelekwa kwenye mahakama kuu ya Nyanza na halafu Mahakama ya Juu zaidi. Hadi hapo pande zote mbili ziliamua kutatua kesi hiyo kwa mawasiliano ya baina yao na wakafikia maamuzi ya kwamba MTN itamlipa mwathirika milioni tatu na nusu za faranga za Rwanda kwa ajii ya fidia (3.500.000 rwf).

Katika ripoti ya wabunge wa tume ya Haki za Kibinadamu bungeni kulibainishwa kwamba MTN Rwanda iliiondoa injini yenye kuleta maafa hayo ila tu haijamlipa mwathirika wa kesi hii ahadi ambayo walifikia kama kupeana kama fidia.

Mwenyekiti wa Tume hii François Byarumwanzi amesema kwamba tatizo linalobaki si la injini za kuwasilisha stima kwenye minara bali kulipwa fidia ambayo walikubali kumlipa.

Wabunge hawakupitisha ripoti hii kwa sababu ya suala hili baada ya kura ya maoni iliyoonyesha idadi pungufu ya ile inayotakiwa.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Walipendekeza suala hili kupelekwa mahakamani badala ya kuletwa mbele ya bunge kwa kuwa maagano yaliyofikiwa kati ya mwathirika na mshitakiwa ambaye ni MTN Rwanda yayakuheshimu sheria kwani angekabidhiwa mahakani kuidhinishwa.

Ripoti hii ambayo haikueleweka kwa wabunge wote ilirudishwa kwa Tume ya Haki za Kibinadamu ya Bunge ili kuifanyiwa marekebisho.

Tatizo la minara limekuwa likijitokeza nchini mwote kwenye siku za hivi karibu ila waziri wa vijana na Teknolojia, Jean Phillibert Nsengimana  alieeleza mwaka jana kwa bunge kwamba vifaa vinavyotumiwa na MTN ni vya kukidhi vigezo kwa Kuwa huwa vimefanyiwa ukaguzi na RURA( Ofisi ya Kukaguwa Huduma na Ubora wa Vifaa kwa ajili ya umma.)

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

Richard Wa Billy

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.