HABARI MPYA

Kamonyi:Nyumba 100 zilizojengwa kinyume na sheria kubomolewa

Gavana wa mkoa wa kusini,Marie Rose Mureshyankwano  ameweka wazi kwamba nyumba 102 zilizojengwa kinyume na sheria zitabomolewa kwa kuwa zimejengwa kwa fujo.

Gavana Marie Rose Mureshyankwano akichunguza ujenzi wa fujo

Diwani mpito wa wilaya ya Kamonyi,Thadee Tuyizere amethibitisha kwa kufafanua kwamba watu waliojenga bila hati au kwa fujo walijulishwa kuhusu jambo hili la kubomoa nyumba zao.

Kwa upande mwingine,watahojiwa viongozi hasa wa kijiji  kuhusu kutotimiza wajibu.

Nyingi mwa nyumba hizi zilijengwa katika tarafa ya Rugalika,Gacurabwenge na Runda.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Maombe
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Most Popular

To Top