kwamamaza 7

Kabuga Felicien miongoni mwa wahalifu wanaotafutwa duniani

0

Orodha hii inatawaliwa na watu mashuhuri duniani kwa uhalifu hususani dhidi ya kibinadamu na kwa vitendo vya kuongoza makundi ya wahalifu ambayo ni hatari kwa usalama wa dunia nzima.

Wengine huwa ni viongozi wa makundi ya kihalifu kama David Ibrahim ambaye ni mkuu wa kundi la D-Company na Joaquìn Guzmàn ambaye anaongoza kundi la Sinaloa Cartel. Kabuga Felicien ambaye ni mnyarwanda anayeshtakiwa uhalifu wa mauaji ya kimbari yumo kwenye orodha hii.

  1. Ayman al-Zawahiri

Ayman al-Zawahiri mtu aliyekuwa kiongozi wa kundi lenye itikadi ya kiislam nchini misri kabla ya kujiunga na Al Qaida iliyokuwa ikiongozwa na Ousama Bin Laden na inasemekana kwamba pia alishiriki shambulizi la kigaidi la 2001 dhidi ya Marekani.

9. Omid Tahvil

Naye ni kiongozi wa kundi la kihalifu la Kanada. Mhalifu mbaya huyu anayeshtakiwa pia kushirikiana na makundi mengine ya kigaidi  alitoroka gereza mwaka wa 2008 na hadi sasa hakuna anayejua alipo.

 8 . Felicien Kabuga

Huyu ni raia wa Rwanda anayeshtakiwa uhalifu unaohusiana na mauaji ya kimbari dhidi ya watutsi ya mwaka 1994. Na anatafutwa na mahakama ili kujibu mashtaka hayo il ampaka sasa yuko ufichoni na hajakamatwa.

7. James Bulger

Ni mwanachama wa kundi la kihalifu la Umarekani mjini Boston, kundi lake pia linafanya linashughulikia na kusafirisha madawa ya kulevya. Anashtakiwa pia kuwaua watu 19. Mhalifu huyu alitoroka polisi na kulingana na biashara yake anamiliki milioni 19 za pauni.

6. Alimzhan Tokhtakhounov

Mhalifu huyu raia wa Urusi anatafutwa kwa mashtaka ya kusafirisha madawa ya kulevya, kufanya biashara ya silaha na hata uhalifu dhidi ya binadamu.

  1. Joseph Kony

Huyu ni raia wa Uganda ambaye ni mkuu wa kundi la waasi wa “Lord Resistance Army” linalojificha misituni DRC, ambalo linashtakiwa, mauaji, uhalifu wa kivita, uhalifu dhidi ya kibinadamu na hata kuwaingiza watoto katika makundi ya waasi.

  1. Semion Mogilevich

Na huyu ni mbaya wa wahalifu raia wa urusi. Ni mkuu wa makundi mbalimbali ya kimafia na anatafutwa sana.

  1. Dawood Ibrahim

Dawood Ibrahim yeye ni mkuu wa kundi la D-Company ambalo linajulikana kwa uhalifu nchini India. Anafanya ulanguzi wa watu na hata kusafirisha madawa ya kulevya

  1. Matteo Messina Denaro

Mhalifu mbaya huyu wa Italia ameshinda miaka mingi akifanya maovu katika makundi ya kimafia na ameshinda miaka zaidi ya 20 bila kugunduliwa.

  1. Joaquìn Guzmàn (El Chapo)

Ni mhalifu mkuu duniani kutoka Mexico na ndiye mkuu wa kundi la Sinaloa Cartel. Kundi hilo linajulikana sana kwa usafirishaji wa madawa ya kulevya, ulanguzi wa watu na makosa mengine. Mhalifu huyu mashuhuri amefahamika kwa kuwa tajiri sana kulingana na biashara hiyo haramu na aliwahi kutoroka Gereza ya California.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Richard Wa Billy

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.