HABARI

Jerusalem ni mji mtakatifu kwa Wakristo,Waislamu na Wayahudi-Papa Francis

Papa Francis ambaye ni kiongozi wa kidini wa wakatoliki wapatao billion moja duniani ametoa maoni yake,akisema kuwa Jerusalem ni mji mtakatifu kwa wakristo,Wayahudi na Waislam.

Pia,Papa Francis ameongeza kuwa mazungumzo pekee ndiyo yanayoweza kuleta suluhu katika mzozo huo wa Israel na Palestina.

Hizi ni fikra ambazo ni kinyume na uamuzi wa Rais wa Marekani, Donald Trump aliyeamua kuwa Jerusalemu ni mji mkuu wa Israel,jambo ambalo linatarajiwa kuzusha ghasia kati ya Israel na Wailamu dunia nzima.

Taarifa za BBC ni kwamba Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Antonio Guterres ametangazia CNN kuwa hatua ya rais Trump kuutambua mji wa Jerusalem kama makao makuu ya Israel inaleta wasi wasi katika jitihada za kuleta amani katika mzozo wa Israel na Palestina.

Pengine,msemaji wa makamu wa rais wa Marekani Mike Pence ameishutumu serikali ya Palestina.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

Maombe
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Most Popular

To Top