kwamamaza 7

Je,Ofisi ya upelelezi wa jeshi ndiyo kizuizi cha ushirikiano kati ya Rwanda na Uganda?

0

Ushirikiano kati ya Uganda na Uganda hauko katika hali nzuri tangu mwaka 2017 hata kama viongozi wa pande mbili hufanya juu chini kuboresha huu ushirikiano.

Kwa maoni yake,chombo cha habari  ambacho hufanya ufuatiliaji wa mambo ya siasa kati ya Rwanda na Uganda,Virunga Post  tarehe 31 Machi 2018 kilitangaza imekuwa kama kawaida ya maafisa wa upelelezi   wa jeshi wa  Uganda(CMI) kuzusha vikwazo wakati ambapo viongozi wa Uganda na Rwanda wangali kuhojiana namna ya kuboresha ushirikiano kati ya Rwanda na Uganda.

Hiki chombo cha habari kilitangaza kuwa ofisi hii inasaidia waziwazi chama cha upinzani kwa serikali ya Rwanda kwa jina la Rwanda National Congress ambao wanaolenga kuishambulia Rwanda ambacho mwenyekiti wake ni Jenerali Kayumba Faustin Nyamwasa.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Kwa kutoa mfano,mwandishi wake ametukumbusha namna ambavyo CMI ilimkamta Mnyarwanda Emmanuel Cyemayire kwa kumshtaki kuwa mpelelezi wa Rwanda wakati ambapo waziri wa mambo ya nje wa Uganda,Sam Kutesa alikuwa nchini Rwanda kwa  niaba ya Rais Museveni kujadili  mambo ya ushirikiano na Rais Kagame.

Pia chombo hiki kimekumbusha namna ambavyo CMI ilimkamata Mnyarwanda mwingine,Claude Iyakaremye baada ya siku mbili ya ziara yake ya kikazi Rais Kagame ambayo ilikuwa ikilenga kuboresha ushirikiano.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Rais Museveni na mwenzake Kagame,walipokuwa Entebbe walikubaliana kuwa mambo ya kuwakamata na kuwatesa Wanyarwanda yatakoma na kuwa suala lolote la  litajadiliwa na pande zote mbili kabla ya utekelezaji.

Kwa upande mwingine,maafisa wa Uganda walitangaza Wanyarwanda waliokamatwa walikuwa na uhusiano na uhalifu wa vitendo vya ugaidi.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Ushirikiano kati ya Rwanda na Uganda ulianza kuwa mkia wa mbuzi tangu mwaka 2017 ambako Uganda ilikuwa ikishtaki Rwanda upelelezi,kuwakamata wakimbizi kinyume na sheria na mengine.Hata hivyo, Rwanda ilikanusha haya madai kwa kusema kuwa Wanyarwanda wanaokamatwa na kuteswa na CMI huwa wanafanya mambo ya kawaida nchini humo.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Subscribe to BWIZA TV to get news and song update

click here to receive the updated news on facebook on twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

[xyz-ihs snippet=”google”]

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.