kwamamaza 7

Jen. Ychaligonza Nduru: wanamgambo wa FDLR wanafuga ng’ombe 

0

Kamanda wa Jeshi kwa Wajibu wa Operesheni Sokola II, Ychaligonza Nduru Jacques amefichua kwamba wanamgambo wa FDLR kutoka Rwanda wanafanyia mambo ya ufugaji wa ng’ombe msituni Virunga.

Tangazo lake limesema wamegundua kuwa FDLR wanafuga ng’ombe 2000 mwezi huu eneo la Kamatembe, Nyamulagira msituni Vurunga.

“ Katika hii operesheni tumegundua kwamba mambo yote ya FDLR yalikuwa yakifanyiwa eneo la Nyamulagira lakini jeshi letu limeyaharibu.” Amesema Jen. Ychaligonza Nduru kupitia tangazo.

Kwa mujibu wa chombo cha habari Actualite,  mwezi Februari 2019 Jeshi la DR Congo (FARDC) lilishtaki FDLR kuwaua wanyama msituni Virunga. Pia, hawa wanamgambo wanashtakiwa kuwaua wananchi 30 eneo la Nyiragongo mwezi uliopita.

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.