kwamamaza 7

Jen. Kale Kayihura afungwa kifungo cha nyumbani kwa amri ya Rais Museveni

0

Wanausalama wamemrudisha nyumbani   kwake Muyenga,mjini Kampala aliyekuwa Mkuu wa Polisi ya Uganda Jen. Kale Kayihura na kumtia kifungo cha nyumbani kwa kutii amri ya Rais Museveni Kaguta.

Kwa mujibu wa Spyreports, Rais Museveni ametoa amri hii baada ya kukutana na watu wengi husika na hili suala wakiwemo kundi kutoka wilayani Kisoro, alikozaliwa Kayihura.

Taarifa hizi zinasema kwamba kayihura amefungiwa kwake lakini anaweza kuwasiliana na wanasheria wake na familia yake.

Pia Kale  Kayihura amepatiwa mfanyakazi wa jikoni

Habari ambazo hazijahakikishwa bado ni kwamba Kayihura atasimama kizimbani baada ya upelelezi wa Bodi Kuu za usalama kama vile CMI na ISO kumalizika.

Jen Kayihura alikamatwa tarehe 13 Julai 2018 kutka Wilayani Lyantonde na kuhojiwa kuhusu masuala tofauti yakiwemo kifo cha Msemaji wa Polisi, AIGP Andrew Felix Kaweesi na uhusiano ulioko kati yake na nchi ya nje ambayo haikutajwa jina.

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.