HABARI MPYA

Jamhuri ya Kongo:Wakimbizi asili ya Rwanda wagoma kurudi nyumbani

Wakimbizi asili ya Rwanda wanaoishi nchini Jamhuri ya Kongo wametangaza kwamba hawatarudi nchini Rwanda kwa kuwa hawamini serilaki ya Rwanda kulinda usalama wao watakaporudi nchini.

Mmoja wao,Dkt.Eric Ndayishimiye ametangazia radiyo sauti ya marekani,idhaa ya Kifaransa kwamba hata kama serikali ya Rwanda ilitangaza kukomesha hali ya ukimbizi tarehe 31 Disemba 2017 hawana nia ya kurudi nyumbani.

Huyu ameongeza kwamba hawana namna nyingine ya kupambana na swali hili isipokuwa kuingia msituni.

Itatubidi kuingia mwituni”amesema Dkt.Eric Ndayishimiye

Pamoja na hayo,waziri wa majanga na mambo ya wakimbizi,Seraphine Mukantabana mwaka jana alitangaza kwamba Mnyarwanda yeyote atakayemaliza mwaka wa 2017 akiwa nje ya nchi,hatakuwa mkimbizi kamwe na kuwa hatapata msaada wa serikali wala UNHCR.

Serikali ya Rwanda ilianzisha mradi wa kuwapatia wakimbizi usafirishaji pia na fedha za kujitunza kwa wazee $250 na watoto $150.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

Maombe
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Most Popular

To Top