kwamamaza 7

Hatua nyingine katika uhusiano wa Rwanda na Israel yapigwa

0

Rais wa Rwanda amepanda mti katika kimsitu cha The Grove of Nations na hiyo ni kuashiria kuimarika kwa Uhusiano wa Rwanda na Israel kwa kuwa mti huo ni ishara ya “Uhai na Amani”.

Paul Kagame amekuwa mkuu wa nchi wa 97 kupanda mti huo wa kuashiria  “Uhai na Amani” ambako siku ya leo akiwa kwenye ziara yake amepanda mti huo wa kuonyesha kwamba Wanyarwanda wana mchango katika shughuli za nchi ya Israel na kuwa uhusiano wao wazidi kupiga hatua.

Mkuu wa Rwanda akihotubia baada ya hafla hiyo amesema kwamba amefurahia hafla hiyo na kwa kuwa mti huo unaashiria mchango wa Wanyarwanda  katika shughuli za Waisrael na ni kielelezo cha historia kati ya Rwanda na Israel.

Licha ya hayo mti huo unakumbusha wajibu wa binadamu kuilinda na kuitunza mazingira hadi kizazi cha miaka ijayo.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Mkuu wa Rwanda alimkuta rais wa Israel Reuven Rivlin kabla ya kitendo hiki.

Paul Kagame aliwahimiza wafanyabiashara na wajasiliamali kuwekeza miradi yao nchini Rwanda kwa kuwa biashara nchini Rwanda iliwafungulia milango watu wa mataifa yote wanaotaka kuendesha biashara kwenye ardhi ya Rwanda.

Nchi hizi zimekuwa na ushiriakiano mzuri kwa miaka ya hivi karibuni na hii inahusishwa na nchi hizi kuwa na historia sambamba za mauaji ya kimbari yaliyozikabili nchi hizi mbili kabla ya nchi ya Israel kuundwa wayahudi wapatao milioni 6 walipoteza maisha katika mauaji ya Kimbari dhidi yao, Rwanda nayo pia ilipitia mauaji ya kimbari dhidi ya watutsi ya 1994 na takriban watu 1994 wakauawa.

Rwanda na Israel zina ushirikiano katika shughuli za kilimo ambako nchi hizo mbili zina kituo cha kilimo ambacho nchi hizo mbili zinachangia kukifadhili. Na wahitimu kuto Rwanda wanasaidiwa kuendelea masomo yao nchini Israel hususani ya kilimo.

Mfumo huu wa kupanda miti katika kimsitu cha The Grove of Nations kilichoko mjini Jerusalem ulianzishwa mwaka wa 2005. Hadi sasa miti mingi imekwisha pandwa na wakuu wa nchi mbalimbali ambao huwa wanaonyesha kuunga mkono mfumo huu . Pia na shirika la UNESCO ambalo hufuatilia mradi huu kwa karibu pia na hata Umoja wa Ulaya.

 

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Richard Wa Billy

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.