HABARI MPYA

Haifai kubomoa nyumba ya mkazi iliyomalizika-Kiongozi wa Transparency International Rwanda,Ingabire Marie Immaculee

Kiongozi wa shilika la kupambana na rushwa na unyanyasaji nchini Rwanda (TI-Rwanda),Ingabire Marie Immaculee ameweka wazi kutokubaliana na uamuzi wa kubomoa nyumba za wakazi zilizojengwa kinyume na sheria uliotolewa na viongozi wa wilaya ya Kamonyi na wa Mkoa wa kusini.

Ingabire Marie Immaculee ametangaza kwamba haifai kubomoa nyumba ya mkazi iliyomalizika kwa kuwa ilijengwa viongozi wa mtaa wakiangalia.

Kiongozi huyu ameongeza kuwa anaona serikali haina budi kuadhibu wasiofuatilia sheria na wale ambao hawatimizi wajibu wao.

Siungi mkono ujenzi wa fujo lakini serikali haina budi kuadhibu pia viongozi badala ya mkazi tu”ameleza Ingabire.

Haya ni baada ya kutangaza kuwa nyumba 100 zilizojengwa kinyume na sheria wilaya ya Kamonyi zitabomolewa.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

Maombe
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Most Popular

To Top