HABARI MPYA

Ghasia gulugulu zazuka kati ya hospitali La Croix du Sud,Abacus na wathiriwa wa anesthesia

Watu watano wameshtaki hospitali ‘La Croix du Sud’ aka ‘Nyirinkwaya’ baada ya kuathiriwa vibaya na anesthesia walizodungwa wakati wa upasuaji mdogo.

Wathiriwa hawa ni Deus Rugigana,Innocent Rubagumya,Schola Mutesi na Angelique Bayitake kwa mijibu wa taarifa za The East African.

Hawa wanaomba fidia ya miliyoni $1.1 kinyume na ile waliyokubaliwa na mahakama ndogo ya Nyarugenge ambayo ilikuwa ni $ 39.076 kutolewa na Abacus Pharmaceuticals.

Kiongozi wa hospitali La Croix du Sud , Jean Crysostome Nyirinkwaya alipokuwa mahakamani alieleza kuwa dawa walizotoa zinakubaliwa na wizara ya maisha.

Pamoja na hayo,wahenga kutoka wizara ya maisha wamesema kuwa hili linahusu na nchi chimbuko la madawa haya.

Hatimaye,maabara mbalimbali yamefanya uchunguzi kuhusu hili,matokeo yalikuwa tofauti kwani Maabara ya Butare na nyingine kutoka Ubelgiji zilithibitisha kuwa anesthesia ili kuwa bandia kinyume na kule Uhindi waligunduwa kwamba anesthesia ilikuwa nzuri kwa maisha.

Mahakama itatoa hukumu tarehe 14 Septemba 2017.

 

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Maombe
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Most Popular

To Top