HABARI MPYA

Gasabo:Viongozi wa ndani waomba rushwa,wakubwa wakapata gao lao

Viongozi wa vijiji kwa majina ya Gaspard(Kira) Munyemana na Wilson Ntakirutimana(Kibenga) katika tarafa ya Ndera wamekamatwa na polisi hapo hapo wakipokea rushwa frw 100,000 ya mkazi kwa jina la Josephine Mukanemeye aliyejenga kinyume na sheria.

Viongozi hawa kwa wajibu wa usalama wamemuambia Josephine uongeza fedha kwani watagawana na viongozi  wakubwa wa eneo na wa tarafa naye akakata kwa kuwa walikuwa wengi sana.

Nilijua kwamba wanayoyafanya ni kinyume na sheria ndiyo maana nimeita polisi”amesema  Josephine.

Mambo ya kugawana rushwa kati ya viongozi yamethibitishwa  na mmoja wa viongozi wa kijiji asiyetajwa majina kwamba katibu mtendaji anazunguka kijiji akichunguza idadi ya nyumba zilizojengwa kisha akamuita kiongozi wa kijiji ili kumpa gao lake la frw 100,000.

Msemaji  wa polisi mjini Kigali,SP Emmanuel Hitayezu amelaumu viongozi wenye tabia mbovu kama hizi na kuwahamasisha kujikosoa ili kutoa mfano mzuri.

Watuhumiwa wamefungwa kwenye kituo cha polisi cha Ndera,mjini Kigali.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

Maombe
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Most Popular

To Top