HABARI MPYA

Uganda: familia sita za Wanyarwanda waliokamatwa zaitaka serikali kutii haki zao

Wanafamilia wa Wanyarwanda waliokamatwa na mafisa wa upelelezi (CMI) tarehe 19 na 20 Disemba 2017 nchini Uganda wamewata viongozi wa jeshi la Uganda(UPDF) kuwafunga wanafamilia wao ama kuwachia huru.

Waliokamatwa kuna Herbert Munyangaju,Freddy Turatsinze,Jessica Muhongerwa,Vanessa Gasaro,Diane Kamikazi na Diane Kamashazi.

Bi Munyangaju, Claudette Ninsiima ametangazia Chimpreports kwamba bwana wake alikamatwa alipokuwa baani mjini Kampala karibu na barabara la Nanyima na kuwa alijaribu na kushindwa kumuona bwana wake alipokuenda kwenye ofisi kuu ya upelelezi.

Pia amesema kuwa kuna taarifa zinazowasababisha wasiwasi kwamba wanafamilia wao wanafungwa kinyume na sheria ,katika hali mbaya pamoja na kuteswa kimwili.

Kupitia wanasheria wao Gawaya Tegulle na Eron Kiiza wameleza kwamba mashtaka ya kuwa wapelelezi na kuwa na uhusiano na vitendo vya ugaidi haina budi kusimama kizimbani siyo kufungwa gerezani.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Maombe
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Most Popular

To Top