kwamamaza 7

Eti Dkt. Frank anastahili kuwa rais wa Sokwe mtu – Wamtukana

0

Dkt. Frank Habineza aliyetangazwa na Tume ya Uchaguzi kama mgombea rasmi wa muda amekabiliwa na matusi kupitia Facebook yaliyoandikwa na mtu anayetambulika kama Chantal Rauch akisema kuwa yeye Dkt. Frank kuwa anastahili rais wa Sokwe mtu.

Dkt. Frank Habineza ambaye ni mgombea kwa tiketi ya chama cha Green alisema atapeleka madai yake kwenye ngazi za polisi kumtafuta mutu huyu aliyemtukana na ili kumpeleka mbele ya sheria. Alisema kuwa kawaida hawana mawasiliano na mtu huyu.

Taarifa hiyi ya facebook ilitangazwa mapema jumatatu ya tarehe 3 mwezi huu ambayo iliandikwa  “Ngewe rwose namufata akaba President ya za Gorilla zacu zo muri Park. Erega nazo zikeneye nk’uriya.” Yenye tafsiri “kwa upande wangu ningemfanya kuwa rais wa gollila wetu wa walio kwenye mbuga ya wanyama. Nao wanamtaka mutu kama yule “

[xyz-ihs snippet=”google”]

Frank baada ya kuiona taarifa hiyi alitoa maoni yake akisema “Imagine this person says I should be president for Gorilla because we look the same. I Hope the government of Rwanda will look into it.” Yaani “Ona mtu huyu kweli anasema napaswa kuwa rais wa Sokwe mtu llila kwa kuwa tunafanana. Nadhani serikali ya Rwanda italifuatilia hili.”

 Frank Habineza alijibu haya kama ubaguzi wa kabila na kuendelea kusema kwamba angehitaji kwaomba serikali ya Rwanda kumtafuta mtu huyu anayetambulika kama Chantal Rauch kwa taarifa alizozichapisha kwenye Facebook.

Akihojiwa Bwiza.com kuonyesha ubaguzi wa kabila ulioko kwenye chapisho lile la facebook alisema “ndio ule ni ubaguzi. Lile lina maana maalum katika siasa ya ubaguzi wa kikabila” aliongeza kwamba mwenye kuchapisha yale alikuwa na makusudi ya kuzua chuki baina ya wanyarwanda.

Kuhusu kuathiri hadhi yake kama mtu mgombea urais alisema kwamba machapisho yale ni ya kumdhalilisha .

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

Richard Wa Billy

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.