KIMATAIFA

DR Congo:Wafungwa 19 watoroka baada ya kubomoa gereza

Wafungwa kumi na tisa, wengi wao wanaokabiliwa na mashtaka ya ubakaji, wametoroka jela mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo usiku wa kuamkia leo, na kusababisha hofu ya kulipiza kisasi kwa waathirika wa vitendo vyao, vyanzo vya serikali za ndani vimesema.

Kwa mujibu wa msimamizi wa gereza Gerard Nkwana, katika jimbo la Kivu Kusini Wafungwa hao 19 walitoroka katika gereza la Kalehe lenye wafungwa 20.

Pascal Nabulera, mkuu wa shirika la kijamii jamii la Kalehe, ametangazia RFI kuwa Watu wanaofika mahakamani kufungua kesi na mashahidi sasa wanawasiwasi wa kulipiziwa kisasi na wafungwa hao waliotoroka.

Nchi ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo yenye umasikini na inayopambana na mgawanyiko wa kisiasa na kikabila pamoja na machafuko mashariki mwa nchi inakabiliwa na matatizo makubwa katika mfumo wake wa mahakama.

Mnamo Mei, wafungwa 4,000 walitoroka katika gereza la Makala huko Kinshasa, mji mkuu, wakati 900 wakitoroka kutoka jela huko Beni katika jimbo la Kivu Kaskazini mwezi Juni.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook n

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Maombe
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Most Popular

To Top