kwamamaza 7

Dkt. Frank kuendesha Kampeni zake kuanzia wilaya ya Rusizi

0

Kampeni za kuania kiti cha Urais wa Rwanda ambazo zinaanza rasmi kesho tarehe ya 14 Julai kwa chama cha Green ambacho Kinaongozwa na Dtk.Frank Habineza kitaanzia kwenye wilaya ya Rusizi.

Kwa mjibu wa habari kutoka mtandao wa twitter Dkt. Frank ataanza shughuli zake za kampeni kwenye kesho tarehe 14 tarehe rasmi ya kuanza kuendesha kampeni kwa mjibu wa ratiba ya Tume ya uchaguzi ya Rwanda NEC. Mgombea huu wa chama cha Green amependa kuanzia kampeni zake kwenye wilaya ya Rusizi ya Jimbo la Magharibi.

Chapisho hilo la twitter liliandikwa “Mgombea kwa tiketi ya DPGR,ataanza shughuli zake za kampeni tarehe 14 katika wilaya ya Rusizi ,Jumamosi tarehe 15 wilaya ya Nyamasheke hatimaye Jumapili tarehe 16 katika wilaya ya Kamonyi”.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Wakati huu wagombea wawili ndio waliokwisha tangaza ratiba ya siku ya kwanza ya kampeni. Isipokuwa Dkt. Frank anayetangaza kwamba shughuli zake za kampeni zitaanza rasmi kesho chama cha RPF nacho kilitangaza hivi majuzi kwamba mgombea wake Rais Paul Kagame ataanzia Shughuli zake za Kampeni kwenye wilaya ya Ruhango ambayo ni wilaya ya kuzaliwa kwake.

Hata hivyo hakuna lolote alilotangaza Mpayimana Phillipe kuhusu kampeni zake mpinzani wao aliyeidhinishwa kama mgombea huru pekee miongoni mwa wengine watatu waliokuwa na mpango wa kuwania kiti cha urais katika uchaguzi wa hapo mwezi Agosti.

Ni mara nyingi Dkt. Frank alizotangaza kuwa yeye atashinda uchaguzi wa rais licha ya kuwa na mpinzani mkali rais Paul Kagame ambaye anaungwa mkono na wananchi kulingana na kuwa walivyoasilisha nyaraka zao kwenye Bunge wakiomba katiba kufanyiwa marekebisho ili Kagame aweze kutawala kwa muhula wa tatu.

 

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Richard Wa Billy

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.