kwamamaza 7

Dkt. Frank aahidi kuleta mabadiliko endapo atashinda uchaguzi

0

Imekuwa ni siku yake ya kwanza ya kampeni ya kuwania kiti cha urais iliyoendeshwa kwenye wilaya ya Rusizi-  Bugarama ambapo amekuwa akifuatiwa na wanachama wake na hasa raia wa kiasi waliokuja kusikia malengo yake.

Katika kampeni yake iliyoanza mnamo saa nane na waliohudhuria ni jumla ya watu wanaokadiriwa kuwa 200 ambao ni  ni pamoja na wanachama wake waliokuwa wakivaa sare ya chama cha Green Party na hawa wakikadiliwa kuwa 30 na watu wengine wanaokadiriwa kuwa 100, na hata raia wengine waliokuja kutega maskio malengo ya mgombea huu na ambao Frank, mgombea wa tiketi ya chama cha Green amesema wanafaa.

Dtk. Akizungumza kuhusu malengo yake amesisitiza kwamba ana imani ya kushinda uchaguzi wa Rais na kwamba atafanya mabadiliko kadhaa endapo atashinda uchaguz. miongoni mwa aliyoyaweka mbele ni ni kufanya mabadiliko kwa sekta ambazo kwake haziendi vizuri kama ubora wa elimu, kuongeza mshahara wa mwalimu, kuziweka sera za kuiendeleza sekta ya kilimo kwa ajili ya kupambana na njaa, na hata kuweka sera za kulinda usalama ambazo zitajumuika na kuweka ndege zisizo na madereva ili kurahisisha kazi ya walinda usalama .

Katika sera zake ameeleza pia kuwa watapunguza kwa kodi na hata kuiondoa kodi ya shamba na mengineyo ambaye ameahidi atawaletea wanyarwanda, na kusisitiza kwamba ana imani ya kushinda uchaguzi kwa aslimia 100 kwamba haiku asilimia 51 kama alivyokuwa akieleza hapo awali.

Amendelea kusema “kuna raia waliokataliwa kuja kujiunga nasi nimeambiwa kuna mahali kulipotokea mambo hayo lakini licha ya hayo mnaona kwamba watu wamehudhuria kwa wingi na hata kura watatupa”

Tutaeneza wangalizi wetu wa kura kwenye vituo vyote vya uchaguzi ili tuweze kuwa na wasimamizi mahali pote ambapo kura zinahesabiwa ili kuhakikisha hatuibiwi kura.

Raia ambao wameongea na Bwiza.com mfano wa Tuyishime Alfred ambaye amesema amekuja kusikia kuhusu malengo ya mgombea huu amesema kwamba amesikia kuhusu malengo ya mgombea huu na kwamba atachukua uamuzi wa nani kumpa kura baada ya kuwasikia wengine.

Raia mwingine ambaye ni mwanachama wa Green, Ntivuguruzwa Sixte, amesema kwamba kwenye chama chake cha Green wana malengo anayoeleweka na ambayo ni muhimu kwa maendeleo ya wanyarwanda na kwa hivyo wana imani ya kushinda uchaguzi.

 

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Richard Wa Billy

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.