HABARI MPYA

Diamond karibu kuanzisha TV na Redio nchini Rwanda

Diamond Platnumz ameeleza mipango ya kuanzisha TV na redio  nchini Rwanda ingali hivi karibuni.

Muimbaji huyo kwenye ziara yake nchini Rwanda kwa ajili ya kuzindua biashara yake amesema kwamba kinachobaki ni kumalizana na vyombo vya sheria.

“Na pia tupo katika harakati za kuhakikisha kwamba ziwe na uwezo wa kufika hadi nchini Rwanda kwa namna moja au nyingine endapo tutamalizana na vyomba vya sheria,” amesema.

Diamond amehakikisha kuwa lengo la Wasafi Fm na Tv ni kuona kwa namna gani vyombo vya habari vinavyoongezeka vinasaidia wasanii kukua kwani kuna wasanii wanajua kuimba lakini hawapati nafasi.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Maombe
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Most Popular

To Top