kwamamaza 7

Dawa ya kumpa adui aliyezuia Baraka zako

0

“Fukua kifusi kilichofukia kisima chako” MWANZO 26;18

Isaka akarudi akavichimbua vile visima vya maji walivyovichimba siku za Ibrahimu babaye; maana wale Wafilisti walikuwa wamevifukia baada ya kufa kwake Ibrahimu; naye akaviita majina kufuata majina alivyoviita babaye.

UOVU ndo KIFUSI….Na kisima chenye CHEMICHEM ya MAJI ni MOYO ULIOFURIKA ROHO MTAKATIFU…Basi ndani yako kuna visima ambavyo vinatoa chemichem ya uzima ikupayo neema.

Toka misingi ya ulimwengu umeadiwa kunywa maji ya kisima chako,lakini adui amekuvizia umelala naye akaja USIKU WA GIZA NENE amevifukia kwa kifusi cha UZINZI/UMASIKINI/UASHERATI/UONGO kila aina ya uovu.Basi leo waambie nimekuja na BULDOZA kuondoa kifusi hicho..Fukua hadi chini kuna chemichem ya Baraka zako..

Maadui walivifukia visima vyako,wakidhani watakukomesha, hawajui una macho ya ndani (ya rohoni) yakupayo matumaini na kujua wapi Vilipo visima vyako ili uvichimbue na kutoa chemichem ya uzima,na hayo maji(ROHO MTAKATIFU) yatabubujika na kukupa uzima wewe na wote walio karibu yako..

Isaka baada ya KUBARIKIWA akakumbuka visima vya baba yake, naye akaanza kufukua kifusi kilichofukia visima ambapo Wafilisti walifukia kabisa na kusahulika..

..UNAPOFANIKIWA utakumbuka zile Baraka ambazo wazazi wako walitakiwa wapate na wewe upate ila adui alizifukia na kuzifunika kabisa….ROHO MTAKATIFU aliye ndani yako atakupasha yaliyopita na yajayo,atakukumbusha PAST na kukujulisha FUTURE yako..

[xyz-ihs snippet=”google”]

Kwani adui huwa anafukia kabisa zile baraka zako ulizopewa na MUNGU toka misingi ya ulimwengu,nawe hujui kuwa KUNA VISIMA VIMEFUKIWA,unajiona unakosa Amani kwakila ukifanyacho kila ukifanyacho akifanikiwi, kumbe adui anakutesa kwakuwa amefukia zile ahadi ulizopewa..Ndani ya kisima chako Kuna kifusi cha uzinzi/uongo/umasikini kila aina ya uovu vyote hivi vimefukia chemichemi yako ndani unajitahidi kufanya mema ya MUNGU huwezi na kukunyima AMANI YA NDANI na kujawa na huzuni..Kifusi ndicho kinachopelekea usimame na kuanguka katika uwokovu wako au usione kabisa faida ya uwokovu.

Unatakiwa kuondoa kila aina kifusi kinachokuzuia mafanikio yako.Kama adui ametumia hicho kifusi kufukia chemichem ikupayo AMANI ya ndoa/mke/mume/mchumba/biashara/ kazi,ili lengo kukufanya usifanikiwe ukose AMANI,leo inakubidi uvifukue kwa JINA LA YESU..

Hivyo vifusi vinazuia Baraka zako,kuna mapepo yamekalia juu hicho kifusi,fukua kwa bidii ili kuyaondoa hayo mapepo,maana kuna vifusi vingine ni vimefukiwa kwa kumwaga ZEGE inahitajika NGUVU ya ziada kuvifukua hivyo vifusi….

Basi ukifukua visima vyako vya ndani ambapo kuna chemichem ya uzima itatoa maji ya Baraka kwako na hayo maji yatamiminika kurudisha UHAI wa ndoa/kazi/biashara/mume/mke navyo vitastawi.

SIKIA kama Kisima kikifukuliwa kwenda chini sana yaani km utafukua ktk kina cha chini kabisa hayo maji(ROHO MTAKATIFU ) yatakayotoka humo kisimani yatabubujika na kumiminika kama mto ambapo utawanywesha watu wengi sana wenye kiu, pindi wakikuona wanapata burudiko la uwepo wako,Na kandokando ya huo mto pia kutastawi hata miti maana vitapata neema kupitia hayo maji(ROHO MATAKATIFU) hivyo vitapata UHAI..

Na maji hayo yatasambaa na kugusa ulimwengu wote yakiwapa UHAI..

Basi ROHO MTALATIFU ndiye asili ya mambo yote,akifurika ndani yako chochote utakachogusa na kutia mkono wako kitastawi na kupata neema.KILA UENDAKO UTAKUWA BARAKA KWA WATU. Nawe ndani yako utakuwa BUBUJIKO la AMANI TELE itiayo UZIMA.

Yatafakari haya yaliyonenwa kisha chukua hatua, maana MEMA yako yalipo wewe wayajua. Mungu wa Mbinguni akufungulie milango yake.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

@bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.