kwamamaza 7

Cristiano ni mchezaji ambaye yupo kwa mechi maalum- Jose Mourinho

0

Meneja wa klabu ya Manchester United, Jose Mourinho amesema kuwa mshambuliaji Cristiano Ronaldo  ni mchezaji ambaye yupo kwa mechi maalum.

Mourinho ameambia chombo cha habari Russia Today kwamba Cristiano ni mchezaji pekee wa mechi maalum.

“Kuna wachezaji wapo kwaajili ya baadhi ya mechi, wengine wapo kwaajili ya kila mechi na kuna wachezaji wao wapo kwaajili ya mechi maalum. Wachezaji ambao wapo kwaajili ya mechi maalum yupo mmoja tu.”

“Ninafahamu hilo na ndiyo sababu ninavutiwa na baadhi ya wachezaji mfano wake,” amesema Mourinho kupitia Russia Today.

“Bao lake la ‘free-kick’ si bora sana ukilinginisha na alicho kifanya Manchester United na alipo jiunga Real Madrid kwa mwaka wake wa kwanza.

“Ni kijana wangu, inauma mimi kusema hivyo lakini anafahamu ni makosa madogo madogo tu lakini kwa kilichotokea ni bora zaidi na kitu kizuri ni kwamba ataendelea kuwepo kwenye mchezo ujao na kamwe wala sihofii hilo.”

Mourinho amefunguka haya  baada ya Cristiano Ronaldo kutupia ‘hat-trick’ na kuisaidia timu yake ya taifa ya Ureno kutoka sare ya mabao 3 – 3 dhidi ya Hispania hapo jana usiku kwenye michuano ya kombe la Dunia.

 Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.