SI KAWAIDA

Chupi ya mke wa Adolph Hitler, Eva Braun yapigwa mnada

Nguo ya ndani ya mke wa Adolf Hitler Eva Braun na vifaa vingine alivyotumia vimeuzwa katika mnada, ambapo chupi iliuzwa kwa pauni 3000.

Chupi hiyo ikiwa ni miongoni mwa vitu vyengine vya bi. Braun ilipigwa mnada katika jumba la mnada la Phillip Serrell huko Melvern ,ikitarajiwa kuvutia pauni 400 lakini ikauzwa kwa pauni 2,900.

Pete ya dhahabu na kiboksi chenye kioo kilichokuwa na lipstiki nyekundu ya Eva Braun pia kiliuzwa.Vyote hivyo viliuzwa kwa mtu binafsi.

_92306926_evaspants

Chupi iliovaliwa na mwenyewe Eva Braun, mke wa Adolph Hitler

Suruali hiyo ilikuwa na kamba ilikuwa na mapambo ya herufi za Eva Braun.

[ad id=”72″]

Pete ya dhahabu iliozungukwa na madini iliuzwa kwa pauni 1,250 huku lipstiki hiyo ya rangi ya fedha ikiuzwa kwa pauni 360.

Wakati huohuo picha za rangi nyeupe na nyeusi za Eva Braun na Adolf Hitler ziliuzwa kwa pauni 100. Wanaoendesha mnada huo wamethibitisha kuwa ziliuzwa kwa mtu binafsi kutoka Uingereza.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

@Bwiza.com

Maombe
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Most Popular

To Top