kwamamaza 7

Burundi kushtaki Rwanda juu ya kuvuruga familia za raia wake

0

Serikali ya Burundi imeahidi itashtaki  Rwanda juu ya kuvuruga familia za Warundi waliokuwa wakiishi nchini Rwanda.

Msemaji wa serikali ya Burundi,Philippe Nzobonariba ameeleza suala la kuwafukuza Warundi nchini Rwanda lilifarakanisha watoto na wazazi wao, wanawake na wanaume wao waliofunga ndoa na Wanyarwanda.

“ Viongozi wa Rwanda hawana budi kujibu suala la kufarakanisha watoto na wazazi wao, wanawake na wanaume wao”

Mmoja mwa waliofukuzwa nchini Rwanda,  Marie Mukerandanga amesema aliwaacha wanawe sita nchini Rwanda.

“Viongozi wa Rwanda walituamuru kuishi katika kambi ya wakimbizi, mimi nikachagua kurudi kwetu kwani sikukimbia nchi. Nilikuwa nchini Rwanda kwa ajili ya kazi”

“Nataka kurudi nchini Rwanda kwa kujali familia yangu” mwingine aliyemuacha mtoto wa miaka miwili ametangazia Iwacu Burundi.

Nzobonariba amesema kuna imani kwamba mashilika ya kimataifa yatasaidia hizi familia zilizovurigika.

Serikali ya Burundi imesema tangu mwezi Juni,Warundi elfu tatu walifukuzwa nchini Rwanda juu ya kugoma kuishi katika kambi za wakimbizi

Rwanda ilitangaza inawafukuza  Warundi ambao hawana vitambulisho rasmi vya kuishi nchini Rwanda.

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.