HABARI

Borussia Dortmund imemfanya Ousmane Dembele mchezaji wa pili ghali duniani(imeboreshwa)

Boruissia Dortmund imekubali ombi la Barcelona kumununua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 anayeaminika kuwa na thamani ya Yuro milioni 100, mapema mwezi Agosti huku mchezaji huyo akipigwa marufuku kwa kukosa kufika mazoezini.

Ousmane Dembele mchezaji wa Borussia Dortmund

Kitita hicho hata hivyo kinakadiriwa kuwa chini ya Yuro milioni 222 ambazo PSG iliilipa Barcelona kumununua Neymar mnamo mwezi Agosti.

Hata hivyo kitita hicho kitakipiku kile kilichotolewa na Manchester United kumnunua Paul Pogba kutoka Juventus.

Mchezaji wa Ufaransa Dembele hajaichezea Dortmund tangu kombe la Supercup mnamo tarehe 5 Agosti 2017.

Amejiunga na Barcelone baada ya kujiunga na Dortmund (Bundesliga) kutoka klabu ya Rennes kwa Yuro milioni 15 miezi 12 iliopita akiwa ameanza kucheza mwaka 2015.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Maombe
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Most Popular

To Top