kwamamaza 7

Bin Rais Museveni amzuru kisiri alipofungiwa Jen. Kale Kayihura

0

Bin Rais Museveni  Jen. Kainerugaba Muhoozi amemzuru kisiri Jen.Kale Kayihura alipofungiwa Makindye mjini Kampala.

Kainerugaba ambaye ni mshauri wa baba yake kuhusu operesheni sizio za kawaida jumanne alimtembelea Jen. Kayihura  kisiri na kukaribishwa na kiongozi  Kanuni William Bainomugisha

Taarifa za Chimpreports  ni kwamba mmoja mwa maafisa wa jeshi ambaye hakutangazwa jina lake amesema mazungumzo ya hawa wawili yalikuwa ya saa mbili.

“ Muhoozi alimkuta Kayihura kwa mazungumzo binafsi” amesema

“Hili lilitokea wakati wa saa moja”

Hata hivyo, huyu hakutangaza nini kilichozungumziwa kati yao.

Hili ni baada  ya nduguye Rais Museveni, Jen. Salem Saleh kumzuru Kayihura.

Jen. Muhoozi alikuwa akifanya kazi pamoja na Jen. Kayihura katika opersheni nyingi nchini Uganda

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.