kwamamaza 7

Arusha:Mahakama yaitaka Rwanda kufunguka kuhusu uamuzi wa kumuachia huru Kanuni Simba Aloys

0

Jaji wa Mahakama ya TPIR huko nchini Tanzania ,Theodor Meron ameandikia barua serikali ya Rwanda akiitaka kutoa maoni yake kuhusu uamuzi wa kumuachia huru Kanuni Aloys Simba ambaye ni mfungwa wa uhalifu  wa mauaji ya kimbali dhidi ya Tutsi 1994.

Hii mahakama imetangaza kwamba Simba Aloys aliandika barua akiomba kuachiwa huru kwa kuwa anamaliza 2/3 za hukumu ya miaka 25 aliyohukumiwa  mwaka 2005.

Jaji Meron ametangaza kuwa  uchunguzi alioufanya pamoja na mwandishi wa kesi ni kwamba Kanuni Simba atamaliza 2/3 za adahbu  tarehe 27 Julai 2018.

Pia,huyu jaji amekumbusha Rwanda kuwa sheria zinakubalia mfungwa aliyeonyesha nidhamu nzuri ambaye anamaliza 2/3 za adhabu kuachiwa huru na kuwa Simba ana matatizo ya afya ambayo yanaweza kumtia hatarini anapoendelea kuishi gerezani.

Taarifa za Sauti ya Marekani zimeeleza  Jaji Meron ameitaka Rwanda kufunguka kuhusu hili jambo kabla ya tarehe 10 Meyi 2018 na kumuomba Aloys Simba kutoa maoni yake baada ya siku 10 hata kama Rwanda imesema chochote.

Kwa sasa,Rwanda haijasema lolote husika ila Tume ya Kupambana na mauaji ya kimbali nchini Rwanda(CNLG) ililaani mambo haya ya kuwaachia huru wafungwa wa uhalifu wa mauaji ya kimbali  kwa kuyalinganisha na  upuuzaji wa mauaji ya kimbali dhidi ya Tutsi.

Simba Aloys,80, alizaliwa kusini magharibi mwa nchi ambako alikuwa na hatia ya kushiriki katika mauaji ya kimbali huko Butare na Gikongoro.

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.