kwamamaza 7

Ambayo mnataka kuyafikia kwa kushirikiana tutayafikia- Paul Kagame

0

Ikiwa leo ni siku ya pili ya kampeni kwa wagombea urais, Paul Kagame ambaye ni mgombea kwa tiketi ya chama tawala cha RPF amekuwa akiendesha akampeni zake kwenye wilaya ya Nyaruguru na Gisagara ambapo amewaahidi kwamba wanayotaka watayafikia iwapo atachoaguliwa.

Alipotoka wilaya ya Nyaruguru aliendelea kwenye wilaya ya Gisagara ambapo amewakuta umati wa waungamkono walipokuwa wakimngojea kwa hamu.

Alipofika kwenye kiwanja cha Ndora ambapo kulikuwa kumejumuika umati alizuunguka umati huu kwa kuwasalimu kwa mikono na maneno yaliyosikika ni “manamtaka nani?” na sauti zikajibu “Paul Kagame”

Akihotubia aliaanza kwa kuwasalimu raia wa Gisagara na kuwaambia kwamba namna wanavyomtaka ndivyo anavyowataka. Aliendelea kuwaahidi kwamba atawafanyia yote wanayotaka, yote kwa kushirikiana, kwa kusaidiana wataendelea kwa kasi.

Kama alivyosema jana akiwa wilaya ya Ruhango aliwashkuru vilevile wanachama wa RPF kwa kuwa na imani na yeye na kumchagua kama mgombea wa tiketi yake.

Aliwaonyesha pia yale ambayo yalifikiwa wilayani Gisagara kama umeme na kusema kwamba licha ya kuwa wanao huduma ya umeme katika wilaya hiyo wangali wanahesabiwa kwa asilimia 22 wanaweza kufika asilimia 100 kila yeyote akawa na umeme.

Rais Kagame aliwafafanulia waliohudhuria hafla hiyo kwamba kuwapa viongozi kura ni kuwapa deni la uadhifa ambalo hawana budi kulipa kwa raia waliowapa kura zao.

Hakukosa kuwaambia raia hao kwamba wana usalama kamili ambapo mnyarwanda analala bila kushtuzwa na hofu ya chochote. Kwa hivyo amewakumbusha wajasiliamali kuweka bidii kwenye shughuli zao na kujiendeleza na hata nchi yao kwa kuwa serikali inawaunga mkono la sivyo hawana la kusema.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Kwa kutamatisha hotuba yake imekuwa ni fursa ya kuwakumbusha raia hao kuwa tarehe 4 Agosti ndiyo tarehe ya kuhakikisha kwamba yale waliyomuomba kupitia kura ya maoni yanafikiwa kwa kumpa kura.

Paul Kagame ataendea na shughuli za kampeni kesho Jumapili tarehe 16 kwenye wilaya tatu ambazo ni Nyamagabe, Huye na Kamonyi.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Richard Wa Billy

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.