kwamamaza 7

Ajali mbili kwa waliokuwa wakienda kushiriki kampeni za RPF -Bazivamo miongoni mwa manusura 65

0

Ajali mbili zatokea kwa waliokuwa wakienda kushiriki kampeni za mgombea wa RPF,ambazo ni pamoja na ya gari alilokuwemo makamu mwenyekiti wa chama cha RPF na nyingine ya Gari la kampuni ya uchukuzi wa abiria ya RITCO Ltd.

Ajali ya gari alilokuwemo Bazivamo imetokea asubuhi ya leo wilaya ya Nyagatare wakati alipokuwa akienda kushiriki kampeni za mgombea wa chama cha RPF Paul Kagame

Kwa mjibu wa habari zilizotangazwa na CIP Emmanuel Kabanda msemaji wa polisi idara ya usalama wa barabara ajali hii ilitokana na uzembe wa dereva wa gari hilo.

Picha ya gari la Bazivamo inazidi kuenea kwenye mtandao wa kijamii lililoanguka kwenye mfereji wa kando ya barabara.

Ajali nyingine iliyotokea ni ya gari ya Kampuni ya kuchukua abiria ya RITCO ambayo imetokea kwenye wilaya hiyohiyo na kuwafanya watu wapatao 30 mwa 65 waliokuwemo kujeruhiwa .

Ajali hii ilitokea kwenye saa za asubuhi kwenye tarafa ya Matimba wilaya ya Nyagatare na kwa majariwa hakuna mtu aliepoteza maisha na waathirika walipelekwa moja kwa moja hospitali. Abiria wa gari hili wote walikuwa wakienda kwenye kampeni za mgombea urais wa chama cha RPF.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Kuna habari zinazosema kuwa ajali hii ilitokana na hali ya uchovu aliyokuwa nayo dereva wa gari hilo.

Hali ya usalama emekuwa nzuri tangu kampeni za uchaguzi kuanza kwa mjibu wa habari zinazotolewa na Polisi ya Rwanda na ajali hizi zinatokea zikiwa za kwanza tangu wakati huo.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Richard Wa Billy

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.